Luke 21:25-33

Kuja Kwa Mwana Wa Adamu

(Mathayo 24:29-35; Marko 13:24-31)

25 a “Kutakuwa na ishara katika jua, mwezi na nyota. Hapa duniani, mataifa yatakuwa katika dhiki na fadhaa kutokana na ngurumo na misukosuko ya bahari. 26 bWatu watazimia roho kutokana na hofu kuu na kuyaona yale mambo yanayotokea duniani, kwa maana nguvu za angani zitatikisika. 27 cWakati huo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni pamoja na uweza na utukufu mkuu. 28 dMambo haya yatakapoanza kutendeka, simameni na mkaviinue vichwa vyenu, kwa sababu ukombozi wenu umekaribia.”

29 eAkawaambia mfano huu: “Uangalieni mtini na miti mingine yote. 30Inapochipua majani, ninyi wenyewe mnaweza kuona na kutambua wenyewe ya kuwa wakati wa kiangazi umekaribia. 31 fVivyo hivyo, myaonapo mambo haya yakitukia, mnatambua kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia.

32 g “Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. 33 hMbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”

Copyright information for SwhNEN